Tofauti Za Mtindo Katika Riwaya Ya Upelelezi Ya Kiswahili: Ulinganisho Wa Mohamed Said Abdulla Na Erick James Shigongo


  • Department: African Studies
  • Project ID: AFS0014
  • Access Fee: ₦5,000
  • Pages: 127 Pages
  • Reference: YES
  • Format: Microsoft Word
  • Views: 484
Get this Project Materials

SHUKRANI

Kwanza kabisa ninatoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu ambaye amenijalia uhai, afya ya roho na mwili na ufahamu wa kuniwezesha kufanya kazi hii. Kuna michango na miongozo ya watu mbalimbali walioniwezesha kukamilisha tasnifu hii. Ninawashukuru wote walionisaidia mpaka kufikia hapa. Ningependa niwataje wote, lakini nitawataja baadhi tu ambao michango na miongozo yao imejitokeza zaidi. Dokta Elias M. Songoyi anastahili kupewa kipaumbele miongoni mwa watu walioniwezesha kufanya kazi hii. Huyu ndiye msimamizi wa utafiti wangu. Licha ya kukabiliwa na majukumu mazito ya kiofisi na kifamilia, ninakiri kwamba alinionesha ushirikiano wa hali ya juu katika maandalizi ya tasnifu hii. Aliweza kusoma kwa wepesi sehemu mbalimbali za tasnifu, kufanya marekebisho kwa upendo, staha na heshima nilipokosea. Kwa hakika, upendo wake ulinisaidia kunipa nguvu na ari ya kuendelea na kazi japokuwa kazi ilionekana kuwa ni ngumu. Aidha, nawashukuru wahadhiri wote tuliokuwa nao pamoja wakati wa masomo kwa misaada yao ya kitaaluma, maelekezo na ushauri kwa muda wote wa darasani ulioniwezesha kukamilisha mafunzo haya. Miongoni mwao ni Prof. J.S. Madumulla, Prof. V. Lakshmanan, Dkt. M. S. Khatibu, Dkt. R. Y. Sebonde na Bwana A. Ponela. Ninaushukuru pia uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma kupitia Kurugenzi ya Masomo ya Uzamili kwa kunidahili na kunipa kibali cha kufanya utafiti katika maktaba za Vyuo Vikuu vya Mt. Augustino, Dodoma na Dar es Salaam. Shukrani zaidi ziende kwa Prof. Mugyabuso Mulokozi na Bwana Wanjala ambao walikuwa ni wakuu wa idara za Kiswahili katika asasi za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mt. Augustino kwa ushirikiano mkubwa walionipa wakati wa utafiti iv wangu. Hawa walinisaidia bila hiana nilipowaomba ridhaa ya kutumia makavazi ya idara zao kwa ajili ya unukuzi na udurusu. Vilevile ninawashukuru wanafunzi wote wa Chuo Kikuu cha Dodoma wa shahada ya uzamili mwaka 2012/2014 na hasa wale wa Fasihi ya Kiswahili kwa ushirikiano na upendo walionionesha tangu mwanzo hadi mwisho wa mafunzo haya. Mwisho kabisa naishukuru familia yangu kwa ushauri na misaada yao ya hali na mali waliyonipa katika kipindi chote kigumu cha masomo tokea mwanzo hadi mwisho. Bila kumsahau dada yangu mpenzi Suzana Alex Chagaka aliyechukua jukumu la kunilelea watoto wagu kwa kipindi chote nilipokuwa masomoni. Mungu aliye mkarimu awazidishie roho ya ukarimu na upendo. Kwanza kabisa ninatoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu ambaye amenijalia uhai, afya ya roho na mwili na ufahamu wa kuniwezesha kufanya kazi hii. Kuna michango na miongozo ya watu mbalimbali walioniwezesha kukamilisha tasnifu hii. Ninawashukuru wote walionisaidia mpaka kufikia hapa. Ningependa niwataje wote, lakini nitawataja baadhi tu ambao michango na miongozo yao imejitokeza zaidi. Dokta Elias M. Songoyi anastahili kupewa kipaumbele miongoni mwa watu walioniwezesha kufanya kazi hii. Huyu ndiye msimamizi wa utafiti wangu. Licha ya kukabiliwa na majukumu mazito ya kiofisi na kifamilia, ninakiri kwamba alinionesha ushirikiano wa hali ya juu katika maandalizi ya tasnifu hii. Aliweza kusoma kwa wepesi sehemu mbalimbali za tasnifu, kufanya marekebisho kwa upendo, staha na heshima nilipokosea. Kwa hakika, upendo wake ulinisaidia kunipa nguvu na ari ya kuendelea na kazi japokuwa kazi ilionekana kuwa ni ngumu. Aidha, nawashukuru wahadhiri wote tuliokuwa nao pamoja wakati wa masomo kwa misaada yao ya kitaaluma, maelekezo na ushauri kwa muda wote wa darasani ulioniwezesha kukamilisha mafunzo haya. Miongoni mwao ni Prof. J.S. Madumulla, Prof. V. Lakshmanan, Dkt. M. S. Khatibu, Dkt. R. Y. Sebonde na Bwana A. Ponela. Ninaushukuru pia uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma kupitia Kurugenzi ya Masomo ya Uzamili kwa kunidahili na kunipa kibali cha kufanya utafiti katika maktaba za Vyuo Vikuu vya Mt. Augustino, Dodoma na Dar es Salaam. Shukrani zaidi ziende kwa Prof. Mugyabuso Mulokozi na Bwana Wanjala ambao walikuwa ni wakuu wa idara za Kiswahili katika asasi za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mt. Augustino kwa ushirikiano mkubwa walionipa wakati wa utafiti iv wangu. Hawa walinisaidia bila hiana nilipowaomba ridhaa ya kutumia makavazi ya idara zao kwa ajili ya unukuzi na udurusu. Vilevile ninawashukuru wanafunzi wote wa Chuo Kikuu cha Dodoma wa shahada ya uzamili mwaka 2012/2014 na hasa wale wa Fasihi ya Kiswahili kwa ushirikiano na upendo walionionesha tangu mwanzo hadi mwisho wa mafunzo haya. Mwisho kabisa naishukuru familia yangu kwa ushauri na misaada yao ya hali na mali waliyonipa katika kipindi chote kigumu cha masomo tokea mwanzo hadi mwisho. Bila kumsahau dada yangu mpenzi Suzana Alex Chagaka aliyechukua jukumu la kunilelea watoto wagu kwa kipindi chote nilipokuwa masomoni. Mungu aliye mkarimu awazidishie roho ya ukarimu na upendo.

  • Department: African Studies
  • Project ID: AFS0014
  • Access Fee: ₦5,000
  • Pages: 127 Pages
  • Reference: YES
  • Format: Microsoft Word
  • Views: 484
Get this Project Materials
whatsappWhatsApp Us